Skip to main content
  • MSD Yakabidhi Vifaa Tiba vya Mil. 500 - Hospitali ya Wilaya Kisemvule

    SERIKALI  kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 500 kwa hospitali ya Wilaya ya Ilala (Kivule), lengo ni kuboresha hali ya utoaji huduma wilayani humo.

    Vifaa hivyo ni pamoja na Vitanda vya kulalia wagonjwa, ventileta za ICU, viti mwendo, friji za kuhifadhia damu na sampuli, vitanda vya uchunguzi, Sunction machine, Ultra Sound machine, magodoro na mashuka.

  • Dkt. Mollel Apongeza Maboresho ya Huduma za MSD

    MTWARA.

    NAIBU Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema ameridhishwa na mabadiliko yanayofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) hususani katika utendaji na utekelezaji wa mikataba ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini.

    Dk. Mollel amesema hayo jana mkoani Mtwara katika ziara ya kikazi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. John Jingu walipotembelea ofisi za Bohari ya Dawa Kanda ya Mtwara, kujionea hali ya utoaji wa huduma na changamoto ya ufinyu wa ghala unaoikabili kanda hiyo.

  • MSD Yabainisha Mikakati Yake kwa Mwaka 2023/2024

    Bohari ya Dawa (MSD) imebainisha kwamba katika Mwaka wa Fedha 2023/24, inatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya zikiwemo dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kupitia mikakati maalumu iliyowekwa na Bohari hiyo.

  • Maboresho ya Mnyororo wa Usambazaji Bidhaa za Afya Nchini

    Ongezeko la usambazaji wa bidhaa za afya unaofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) tangu Mwaka wa Fedha 2022/23 baada ya mapitio ya mnyororo wa ugavi na mapendekezo ya maboresho ya usambazaji bidhaa za afya, umepelekea kuimarika kwa upatikanaji wa bidhaa hizo nchini.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.