Skip to main content
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya  Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilaya ya Kilombero Wakishiriki Kupakua Bidhaa za Afya Kutoka Kwenye Lori la MSD, Lililoleta Bidhaa za Afya Wilayani Humo

Serikali Yakabidhi Vifaa Tiba vya Milioni 900 Halmashauri ya Ifakara

#MOROGORO

SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 900 kwa Halmashauri ya Ifakara mji.

Akizungumza jana Mkoani humo, Mbunge wa Kilombero Mhe.Abubakar Asenga, alisema ujio wa vifaa hivyo, utasaidia kuboresha huduma za afya hivyo wanaishukuru serikali kwa hatua kubwa ya maboresho katika sekta hiyo.

Alieleza kuwa, jimbo hilo lilikuwa na kero saba muhmu na kubwa ambazo hazijawahi kutatuliwa tangu kupata Uhuru lakini Rais Dk. Samia amezitatua ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara, maji, ukarabati kituo cha umeme Kidatu,ujenzi wa shule za kata, vituo vya afya, zahanati na hospitali.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya amesema ujio wa vifaa tiba hivyo ni neema kwa halmashauri hiyo.

Alisema, maboresho hayo makubwa yanayofanywa na Rais Dk.Samia ni lazima kuungwa mkono na watendaji hivyo anatoa siku 15 kuhakikisha MSD inafunga vifaa hivyo na wananchi wanaanza kupata huduma.

“ Niwaombe MSD ilete wataalamu wao kwa ajili ya kufunga vifaa hivi, haiwezekani Rais wetu afanye mambo makubwa kama haya watendaji tumuangushe, ni muhimu kuhakikisha tunasimamia na wananchi wanaanza kupata huduma kwa wakati,”alisema.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa MSD ambaye ni Mfamasia na Afisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam Diana Kimario, alisema kanda hiyo ina hudumia mikoa mitatu ambayo ni Dar es salaam, Pwani, Morogoro ambapo Ifakara ni mnufaika.

“Ujio wa vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 900 ni muendelezo wa mabadiliko makubwa katika maboresho sekta ya afya, sisi watumishi ndani ya MSD tunajivunia namna serikali yetu chini ya Rais Dk. Samia, Waziri wetu wa afya Mhe. Ummy Mwalimu na Mkurugenzi wa MSD Mavere Tukai wanavyohakikisha tunafanya kazi kwa weledi.

Aliongeza kuwa kama MSD, wamejipanga kupitia maboresho ya ndani, ikiwemo mikataba, ili kuhakikisha Dawa na Vifaa tiba vinapatikana kwa wakati, na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.