Skip to main content
  • Katibu Mkuu Afya, Aitaka MSD Kuwajali Wateja Wake

    Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu ameilekeza Bohari ya Dawa (MSD) kuwajali wateja na kuwashirikisha katika suala zima la kuwapa huduma za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za Afya nchini.

    Dkt. Jingu amesema hayo wakati  akifungua kikao cha ishirini na mbili  (22) cha baraza la Wafanyakazi la MSD Mkoani Morogoro ambapo amesisitiza kuwa, kujali wateja ni msingi wa kuwahudumia kulingana na mahitaji yao.

  • MSD Yakabidhi Vifaa Tiba vya Mil. 114 - Kituo cha Afya Mtae

    SERIKALI imetoa Sh.Milioni 114 kwa Kituo cha Afya  Mtae kilichopo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ambazo zimetumika kununulia vifaa tiba kupitia Bohari ya Dawa (MSD) na hivyo kinatarajia kuanza kutoa huduma ya upasuaji mwishoni mwa mwezi Disemba 2023.

  • Rais Samia Afunga Kazi Sekta ya Afya - Wilaya ya Mvomero

    RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amefunga kazi Mvomero kwa serikali kukabidhi dawa na vifaa tiba vya zaidi ya sh. bilioni 1.61.

    Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judithi Nguli wakati Bohari ya Dawa (MSD), ilipokabidhi dawa na vifaa tiba vya zaidi ya sh. bilioni 1.61 kwa vituo vya afya na hospitali za wilaya hiyo.

  • Serikali Kupitia MSD Kanda ya Dar es Salaam Yasambaza Vifaa Tiba vya Milioni 930 - Wilaya ya Ulanga.

    SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dar es Salaam imesambaza vifaa tiba vya zaidi ya sh. milioni 930 kwa ajili ya vituo vya afya 24 vya halmshauri ya Wilaya ya Ulanga.

    Akizungumza jana Wilayani humo mkoani  Morogoro Mbunge wa jimbo la Ulanga Salim Hasham, alisema, wamepokea vifaa tiba hivyo na dawa za zaidi ya sh. milioni 900 kwa ajili ya vituo vya afya 23 vya halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.

  • Rais Samia Apeleka Tabasamu Kwa Wananchi wa Kata ya Magazini - Wilaya ya Namtumbo

    Kituo cha Afya cha Magazini kilichopo Kata ya Magazini  Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma  kimepata msaada wa vifaa Tiba vya kisasa vya upasuaji vikiwemo vya wamama wajawazito  vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 100 ili  kuweza kusaidia kuboresha huduma za afya kwenye kata hiyo, iliyoko mpakani na nchi ya msumbiji .

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.