Ruka kwenda maudhui makuu

Watumishi wa MSD Wafanya Ziara ya Kikazi katika Wakala wa Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMSA)

Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) kutoka Kitengo cha Maoteo wamefanya ziara ya kikazi katika Wakala wa Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar (CMSA), kwa lengo la kujionea jinsi huduma za MSD zinavyochangia uendeshaji wa taasisi hiyo, na kujadili kwa pamoja changamoto za kiutendaji ili kuboresha huduma kwa wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CMSA, Bi. Lulu Sheikh Abdulrahman, alisema taasisi yake inafurahia ushirikiano wa muda mrefu na MSD katika nyanja mbalimbali, ikiwemo Mkataba wa Maridhiano (MOU) unaoiruhusu CMSA kuagiza dawa kutoka MSD.

Aliongeza kuwa MSD imekuwa ikitoa huduma za kuridhisha, hali iliyowezesha CMSA kununua baadhi ya dawa kutoka kwa Bohari hiyo.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Maoteo MSD Bw.Oscar Tenganamba alisema ziara hiyo imeongeza ari ya kuendeleza ushirikiano, hasa katika eneo la maoteo ya bidhaa za afya, nakusisitiza kuwa MOU iliyopo baina ya pande hizo mbili itaendelea kutumika kuhakikisha bidhaa za afya zinazoombwa na CMSA zinawasilishwa Zanzibar kwa wakati, kama makubaliano yanavyoelekeza.

Kupitia ziara hiyo, ujumbe huo kutoka MSD pia ulipata fursa ya kutembelea ghala la dawa la CMSA na kujionea jinsi bidhaa za afya zinavyohifadhiwa.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.