Ruka kwenda maudhui makuu

MSD Yaongeza Kasi ya Ushirikiano na Wadau, Yahitimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa Ziara Maalum

Bohari ya Dawa (MSD) imehitimisha Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 kwa kufanya ziara maalum kwenye mabanda ya maonesho ya wadau na wateja wake, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Zoezi hilo limeongozwa na Meneja wa Rasilimali Watu , Hans Mwambuba, pamoja na Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma Mwanashehe Juma, ambapo walitembelea taasisi mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Katika mazungumzo yaliyofanyika, viongozi wa MSD walieleza hatua zinazochukuliwa na taasisi katika kuimarisha utendaji kazi, hususan katika usambazaji wa bidhaa za afya, pamoja na kuhakikisha watumishi wake wanatekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Kwa upande wao, viongozi wa taasisi zilizotembelewa walipongeza ushirikiano wanaoupata kutoka MSD, wakieleza kuwa umechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watumishi na wananchi kwa ujumla.

Wadau hao pia waliahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na MSD, ikiwemo kufanya maoteo sahihi ya mahitaji ya vituo vyao vya huduma, hatua ambayo itasaidia kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana wakati wote na kuepusha changamoto ya upungufu wa bidhaa za afya.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamekuwa fursa muhimu kwa MSD kuimarisha mawasiliano na wadau wake, kusikiliza maoni yao na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu majukumu na mchango wa taasisi hiyo katika sekta ya afya nchini.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.