Prof. Makubi Apiga Marufuku Kulipisha Gharama za Chanjo

KATIB_1.jpg

              Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi(kulia), Akizindua Usambazaji Chanjo ya UVIKO 19

 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa angalizo kwa wasimamizi wa chanjo kutolipisha watu fedha kwani chanjo hizo ni bure huku akihimiza kuzingatiwa kwa weledi wakati wa zoezi hilo.

 

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu (Afya), Prof. Abel Makubi wakati akizindua zoezi la usambazaji  wa chanjo kwenda mikoa mbalimbali nchini, tukio ambalo limefanyika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jijini Dar es salaam.

 

Prof. Makubi amesisitiza kwamba utoaji wa chanjo hizo kwenye hospitali za Umma na binafsi, utatolewa bila kulipisha gharama za aina yeyote.

 

KTB2.jpg

         Prof. Abel Makubi(kulia), Akionyesha box dogo la Chanjo ya UVIKO 19, mbele ya waandishi wa habari

 

"Naelekeza kwa huu mgao wa Covax Facility ni marufuku Hospitali za umma au binafsi kulipisha Wananchi gharama yoyote katika zoezi hili la chanjo na lifanyike kwa uadilifu na kwa haki kwa walengwa wa sasa." Alisema Prof. Makubi.

 

Ameongeza kuwa, Pamoja na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufanikisha upatikanaji wa chanjo hizo na kuanza kuchanja Wananchi, Wizara ya afya inaendelea kuwashauri Wananchi kujikinga na UVIKO-19.

 

index.jpg

                      Prof. Abel Makubi(kulia), Akitembelea Majokofu yaliyo hifadhi Chanjo ya UVIKO 19

 

"Kwa kuzingatia kanuni za UVIKO 19, tunapaswa kunawa mikono, kuvaa barakoa, kukaa umbali za mita moja au zaidi, kuepuka misongamano na kufanya mazoezi.

 

Aidha, amesema ugawaji wa chanjo umezingatia taarifa ya visa vya wagonjwa waliohisiwa kuwa na UVIKO-19, idadi ya walengwa kwa kundi la kipaumbele pamoja na idadi ya chanjo zilizopatikana kwa sasa.

Mameneja wa Kanda za MSD Wanolewa

1.jpg

                        Mkurugenzi wa Rasilima Watu na Utawala wa MSD, Bw. Erick Mapunda akifungua

                                kikao cha tathimini kilichohusisha Mameneja wa Kanda wa MSD

 

Mkurugenzi wa Rasilima Watu na Utawala wa MSD, Bw. Erick Mapunda amewataka Mameneja wa Kanda za MSD kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu yao ili kufikia lengo la taasisi katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.

 

Bw. Mapunda ametoa rai hiyo leo wakati akifungua kikao kazi cha Memeneja wa Kanda wa MSD waliokutana MSD Makao Makuu kwa ajili ya tathmini ya utendaji ya mwaka wa fedha uliopita, pamoja na kuweka malengo mapya ya mwaka huu wa fedha.


2.jpg

                     Mameneja wa Kanda za MSD, Wakifuatilia mada wakati wa tathimini ya utendaji

Wataalamu Kutoka Muhimbili Watembelea MSD

Z3.jpg

                           

Baadhi ya madaktari na Wataalam wa baabara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Mloganzila

wametambulishwa mashine na vitendanishi vya maabara vipya vinavyonunuliwa na Bohari ya

Dawa(MSD) kwa matumizi ya vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali nchini.

 

Z6.jpg

Mtaalam wa maabara wa MSD Joseph Kitukulu amewaeleza kuwa,mbali na vifaa

hivyo kutumia teknolojia ya kisasa, kupunguza muda na kuwa na gharama nafuu

vinauwezo wa kuchukua sampuli nyingi zaidi.

 

Z2.jpg

Kwa upande wake,Msimamizi wa Utekeleza Mpango Mkakati wa MSD, Bi. Neema

Mwale amesema kuwa hatua ya MSD kununua vifaa hivyo kutoka kwa wazalishaji

itachangia juhudi za serikali kuboresha huduma za afya za wananchi na kuipunguzia

serikali gharama kwa takribani asilimia 40 hadi 50.

 

 

 

Mkurugenzi Mkuu NHIF Aipongeza MSD

PIC_4.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga, ameipongeza MSD kwa kuboresha mfumo wake wa manunuzi ya vifaa vya maabara na vitendanishi vyake, kwa kwenda kununua vifaa hivyo moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji.

Ameongeza kuwa hatua hiyo itarahisha upatikanaji wa vifaa hivyo nchini na kupunguza gharama za huduma za vipimo vya kimaabara kwa wananchi.

 

PIC_1.jpg

Bw. Konga ametoa pongezi hizo alipotembelea Makao Makuu ya MSD kwa lengo la kuboresha uhusiano na ushirikiano wa kikazi baina ya MSD na NHIF, mathalani katika kuboresha huduma za kimaabara kwenye vituo vya kutolea huduma za afya chini.

 

Kwa upande wake Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi wa MSD Bw. Joseph Kitukulu, amesema gharama za vifaa hivyo na vitendanishi zimepungua kwa zaidi ya asilimi 50, ambapo vituo vya kutolea huduma za afya vya ngazi zote nchini wanaweza kuwa navyo.

PIC_2.jpg

 

Aliongeza kuwa vifaa hivyo ni pamoja na mashine ya kupima wingi wa damu, sukari na zile za kupima kiwango cha kemikali mwilini.

Aidha kwa upande wa mashine za kuchuja damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo, mashine zilizonunuliwa zitawezesha kushuka kwa gharama za uchujaji wa damu kwa wagonjwa hao kwa kiasi kikubwa.

Tayari vituo vya afya nchini vimeanza kununua mashine hizo kutoka MSD, huku wataalamu wa maabara wa MSD wakiendelea kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuzitambulisha mashine hizo na kujiridhisha kuhusu utendaji kazi wake.

 

PIC3.jpg


Dkt. Gwajima, Afanya Ziara MSD

DK_Gwajima.jpg

                                                   Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo tarehe 3 mwezi wa 7,2021, amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimentiya Bohari ya Dawa (MSD) Kwenye ukumbi wa Bohari ya Dawa ulioko Keko jiji Dar es salaam, lengo likiwa ni kuangalia namna gani ya kuboresha huduma na upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

 

Dkt. Gwajima licha ya kukutana na Menejimenti ya MSD katika kikao cha ndani, alitembelea kiwanda cha kuzalisha Dawa cha Keko (Keko Pharmaceutical) kilichopo jijini Dar es Salaam, kinachosimamiwa na Bohari ya Dawa (MSD).

 

Katika Ziara hiyo Dkt.Gwajima alijionea uzalishaji wa dawa ambapo hivi Sasa kinazalisha aina kumi za dawa, zikiwemo za maumivu aina mbili na nyingine 8 zikiwa ni dawa za kuua vimelea vya magonjwa ya kuambukiza (antibacteria/antibiotics).

waziri_Gwajima_na_Menejiment.jpg

                         Dkt. Dorothy Gwajima akiwa kwenye kikao cha ndani na Menejimenti ya MSD

Hatahivyo, licha ya kazi kubwa iliyofanyika kiwandani hapo, Dkt. Gwajima alitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa kiwanda hicho, kwaajili ya kuboresha utendaji, uzalishaji, na taarifa muhimu zinazohusu kiwanda hicho.

 

Katika hatua nyinine,Dkt. Gwajima alitembelea Maghala ya kuhifadhia dawa, yaliyoko Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jijini Dar es Salaam, na kuijonea uhifadhi wa dawa, sambamba na changamoto mbalimbali zinazoikumba Bohari hiyo upande wa uhifadhi na kuagiza mabadiliko kwenye maeneo mbalimbali ili kuboresha huduma za usambazaji wa bidhaa za dawa nchini


KIWANDA_KEKO.jpg

Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mej.Gen Gabriel Saul Mhidze

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker