Skip to main content

PSSSF Yaitambua MSD kama Mshirika Muhimu

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF umeitambua Bohari ya Dawa (MSD) kama mshirika muhimu katika kuchangia maboresho ya huduma za mfuko huo. Utambuzi huo umefanywa leo wakati wa hitimisho la wiki ya huduma kwa wateja. PSSSF imekuwa kwenye mahusiano mazuri ya kiutendaji na MSD hasa katika kuhakikisha michango ya watumishi wa MSD inawasilishwa PSSSF kwa wakati kwa kutumia mifumo mbalimbali ya kielektroniki. 

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo ya kutambuliwa Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD Bi. Gendi Machumani amesema zawadi hii inaonesha namna PSSSF inavyothamini uhusiano uliopo baina ya taasisi hizi mbili. Zawadi hii ni uthibitisho wa uhusiano bora uliopo, MSD itaendelea kufanya kazi kwa karibu na PSSSF ili kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wa taasisi hizi.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD was established for the purpose of production, procurement, storage, and distribution of approved health commodities required for use by health facilities. In living this mission, we ensure that health commodities in Tanzania are accessible, reliable, and affordable but also delivered on time at all health facilities in Tanzania and beyond.

Featured Posts

Contact info

Our mission: To make quality health products accessible to all public health facilities in Tanzania.