Skip to main content

MSD Iringa yajadili Maboresho ya Huduma na Wadau Wake, Yatunuku Zawadi

Bohari ya Dawa (MSD) kupitia Kanda yake ya Iringa imetekeleza jukumu muhimu la kijamii kwa kukabidhi msaada wa vifaa tiba na zawadi mbalimbali kwa vituo vya kutolea huduma za afya katika mikoa ya Iringa na Njombe, ikiwa ni hitimisho la maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025.

Miongoni mwa taasisi zilizopokea msaada mkubwa ni Hospitali ya Wilaya ya Wanging’ombe, ambapo MSD ilikabidhi zawadi mbalimbali kwa wadau hao, ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Katika wilaya ya Mufindi, Zahanati ya Igombavanu ilipokea msaada wa mashuka 10, kitanda cha kujifungulia na zawadi mbalimbali kwa ajili ya wahudumu na akina mama wajawazito wanaohudumiwa katika zahanati hiyo. Vifaa hivyo vitasaidia kuboresha mazingira ya kujifungulia na kuinua viwango vya huduma za afya kwa akina mama na watoto.

Katika Hospitali ya Mji wa Mafinga, MSD ilikabidhi mashuka 30 na zawadi mbalimbali, huku Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ikipokea mashuka 50 na msaada mwingine wa zawadi mbalimbali. Vifaa hivyo vinatarajiwa kuongeza faraja kwa wagonjwa na kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizo kubwa.

Kwa ujumla, maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yamekuwa jukwaa muhimu kwa MSD kuonesha dhamira yake ya kuwahudumia wateja kwa ukaribu, kusikiliza maoni yao na kutoa mchango unaoendana na mahitaji halisi ya vituo vya afya nchini.

Aidha, zoezi hilo la utoaji wa msaada limeambatana na mazungumzo ya ana kwa ana kati ya maafisa wa MSD na viongozi wa vituo vya afya, ambapo changamoto mbalimbali zinazohusu upatikanaji wa bidhaa za afya, utaratibu wa uagizaji na usambazaji wa dawa na vifaa tiba zilijadiliwa kwa lengo la kupata suluhisho la pamoja. Hii ni sehemu ya mkakati wa MSD wa kujenga mahusiano imara na wateja wake na kuimarisha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD was established for the purpose of production, procurement, storage, and distribution of approved health commodities required for use by health facilities. In living this mission, we ensure that health commodities in Tanzania are accessible, reliable, and affordable but also delivered on time at all health facilities in Tanzania and beyond.

Featured Posts

Contact info

Our mission: To make quality health products accessible to all public health facilities in Tanzania.