Kanda ya MSD DSM Yakutana na Wateja Wake
Wateja wa MSD kutoka vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam leo wamepata fursa ya kutembelea ghala la kuhifadhia bidhaa za afya la Kanda ya Dar es Salaam na kujionea bidhaa mbalimbali zinazotunzwa na kusambazwa na MSD. Hatua hii imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Akiwakaribisha wateja hao Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Bi. Betia Kaema amesema wiki hii ni muhimu kwa watoa huduma na wateja wao kukaa pamoja na kujadili mambo mbalimbali yanayoweza kuboresha huduma. Bi. Kaema aliongeza kuwa MSD ipo tayari kupokea maoni mbalimbali na kusikiliza changamoto ambazo zinawakabili kipindi cha kupokea huduma zetu ili kuzifanyia kazi.