DKT. Shein Amwaga Pongezi kwa MSD.

DKT_SHEIN.jpg3.jpg

                          Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

                    Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza MSD kwa kuteuliwa

                           kuwa mnunuzi mkuu wa dawa kwa ajili ya nchi za SADC.

 

                                Dkt. Shein alimweleza hayo Mkurugenzi Mkuu wa MSD

                        Laurean Bwanakunu alipotembelea banda la MSD katika maonesho

                                  ya viwanda yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 

                  Kingozi huyo pia ameishauri MSD kuwatembelea wazalishaji wakubwa

                       wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara wa mataifa

                     ili wapate taarifa sahihi na kuwashirikisha kuhusu MSD kuteuliwa

                        kusimamia manunuzi ya pamoja ya dawa kwa nchi za SADC.

 

                           DKT_SHEIN.jpg                               

                          

                     Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu

                   amesema tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya manunuzi ya pamoja,

                   ambapo tayari wameanza mchakato wa kupata wazabuni na kuanzisha

                mfumo wa kielektroniki utakaotumiwa na nchi wanachama kuleta mahitaji.

 

               Bohari ya Dawa MSD, ni moja ya taasisi zilizoshiriki maonyesho ya biashara

              na viwanda ya SADC yaliyofanyika wakati wa wiki ya mkutano wa SADC 2019,

                   katika viwanja vya kimataifa vya Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

MSD Yawasilisha Msaada wa Dharura kwa Majeruhi wa Ajali ya Moto Mkoani Morogoro

MOROGORO_CSR.jpg

                                ,

 

      

                                         Timu ya MSD ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD

                                Bw. Laurean Bwanakunu wakiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Serikali

                                   Prof. Mohamed Kambi, wamewatembelea majeruhi wa ajali ya moto,

                                iliyosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta waliolazwa katika hospitali

                                                             ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

 

                                                                MOROGORO_CSR.jpg4.jpg

 

                                 Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao, ujumbe huo pia ulilenga

                               kufuatilia na kufahamu misaada ya haraka ya kitabibu inayohitajika

                                            kwa sasa hospitalini hapo ili kusaidia majeruhi.

                                                              MOROGORO_CSR.jpg3.jpg

 

                          Aidha, Bohari ya Dawa imechukua jitahada za makusudi kwa kusafirisha

                                shehena hiyo kutoka kwenye magahala yake jijini Dar es salaam,

                                                  ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu.

 

 

 

 


 

Waziri Ummy Mwalimu, Ahimiza Ujenzi wa Viwanda vya Dawa Nchini

5555555555.jpg

                                ,

 

        Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

          amesema serikali inawajengea mazingira mazuri wazalishaji dawa,vifaa tiba na

     vitendanishi vya maabara wanaowekeza nchini kwani wanasaidia kupunguza gharama

                                                za kuagiza dawa nje ya nchi.

 

        Waziri Huyo ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Tatu wa mwaka

        wa wazalishaji na wasambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara

                                       kutoka nchi mbalimbali duniani.

 

7777777777.jpg

 

            Mkutano huo umeandaliwa na Bohari ya Dawa kwa kushirikiana na UNDP

             ambapo mwakilishi wa UNDP Dr. Rosemary Kumwenda amesema mkutano

           huu ni muhimu kwani MSD kwa sasa inafanya kazi kimataifa na UNDP kama

             wakala wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa inawajibu wa kuunga mkono

           jitiada za MSD kuhakikisha shughuli zinazofanywa na MSD zinakuwa na              

                                                  manufaa kwa wananchi.

 

6666666666666.jpg

 

           Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema wameandaa

               mkutano huo ili kuweka mazingira ya uwazi na kuboresha utendaji wa

         MSD na kuwavutia wazalishaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara

                                                        kuja kuwekeza.


 

Waziri Bashungwa Asema Serikali Imeweka Mazingira Rafiki kwa Uanzishwaji wa Viwanda Nchini

waziri_pp.jpg

                                ,

 

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Mhe. Innocent Bashungwa amefungua mkutano

wa kwanza wa kimataifa wa wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba,ulioandaliwa

na Bohari ya Dawa (MSD).

 

Waziri huyo ameeleza kuwa kufuatia sera ya Tanzania ya viwanda, serikali

imewekamazingira rafiki ya uwekezaji wa viwanda vya kuzalisha dawa nchini ili

kuwawezesha wawekezaji wenye nia.

 

Amesema hatua hiyo itapunguza pia utegemezi mkubwa wa dawa na vifaa tiba

kutokanje ya nchi, kwani kwa sasa taifa linapoteza fedha nyingi za kigeni katika

kununulia bidhaa hizo za afya.

 

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema wameandaa mkutano

huo ili kuweka mazingira ya uwazi kupata wawekezaji,ambapo wamewaeleza matokeo

ya utafiti uliofanywa na mshauri mwelekezi wa mradi wa uanzishaji viwanda vya dawa

kwa ubia wa sekta ya umma na sekta binafsi.

 

Wananchi Wilayani Chemba Waipongeza Serikali kwa Kuboresha Huduma za Afya

 

MSD_DRIVER.jpgMSD_CSO.jpg_MG_9426.jpg_MG_9435.jpgMWENYEKITI.jpg_MG_9431.jpg

Wananchi wa Kata ya Sanzawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wameipongeza Serikali kwa kuboresha huduma za afya kuwapelekea dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa wakati jambo ambalo limewaondolea usumbufu wa kupata matibabu wanapoumwa.

Pongezi hizo walizitoa kwa nyakati tofauti wilayani humo wakati wakizungumza na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD), ambao wanawatembelea wateja wao katika vijiji vya Mkutimango na Minyembe kujua changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Mkazi wa Kijiji cha Moto, Ali Tengeneza alisema anaipongeza MSD na Serikali kwa kufanikisha kuwafikishia dawa kwa wakati tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakilazimika kwenda kuzinunua katika maduka ya watu binafsi.

" Watu katika familia yangu wakiumwa huwa nawaleta kutibiwa katika Zahanati yetu hii ya Kijiji cha Sanzawa na hakuna siku waliyokosa dawa " alisema Tengeneza.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Sanzawa, Shabani Msemule alisema hapo awali walikuwa na changamto ya upatikaji wa dawa lakini hivi sasa haipo na dawa zinapo kuwa zimekwisha katika zahanati hiyo huwa wanakwenda kutibiwa Kituo cha afya cha Kwamtolo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji wa zahanati hiyo, Iddi Degera alisema hivi sasa hakuna changamoto ya upatikanaji wa dawa kwenye zahanati hiyo dawa na mahitaji mengine yanayohusu afya yanapatikana.

Mkazi mwingine wa Kata hiyo, Nicholaus Dominick aliiomba serikali kuboresha zaidi miundombinu ya zahanati na vituo vya afya.

Mjumbe wa Kamati ya Afya ya Kijiji hicho, Flaviana Joseph alisema mara kwa mara wamekuwa wakipokea dawa kutoka MSD na kuzipokea kwa utaratibu uliopo na orodha ya dawa zote wanazozipokea na thamani yake hubandikwa kwenye ubao wa zahanati hiyo ili kila mwananchi aweze kuona.

Muuguzi Msaidizi na Mkunga wa zahanati hiyo, Dativa Kiabuka alisema dawa zote muhimu wamekuwa wakizipata kwa wakati na hawajawahi kupungukiwa kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kutoa oda pale wanapoona zinapungua na kuwa katika eneo hilo magonjwa yanayosumbua zaidi ni malaria,kukooa na matumbo na kuwa wagonjwa wanaotibiwa ni kuanzia 20 hadi 50 kwa siku.


 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker